News

SUDANI KUSINI: SALVA KIIR AOMBA RADHI KWA WATUMISHI WA UMA.

on

Raisi wa Sudani ya Kusini Salva Kiir, amewaomba radhi watumishi wote wa uma kwa kushindwa kuwapa mishahara yao kwa wakati na kusababisha kulimbikizwa kwa madeni mengi ya mishahara.

Raisi wa Sudani ya Kusini akilihutubia taifa

Kiir aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo, ikiwa ni mwaka wa 8 tangu kupatikana kwa uhuru nchini humo.

Radio Miraya iliyopo jijini Juba nchini humo, imeripoti kuwa, Raisi Kiir amezielezea sababu za kushindwa kutoa mishahara kwa wakati, ni kutokana na viongozi wachache wanaoshindwa kusimamia majukumu yao, pia ni pamoja na matatizo ya kiuchumi ambayo taifa limekuwa likipitia.

Pia ilielezwa kuwa, mwezi uliopita, waziri wa fedha nchini humo, alishindwa kuwasilisha bajeti ya mwaka, baada ya wabunge kutoka nje ya bunge wakati wakilalamikia tatizo la mishahara kushindwa kulipa kwa wakati.

miaka 8 ya uhuru wa taifa la Sudani ya Kusini, haijasherehekewa kwa shamrashamra, kutokana na matatizo ya kiuchumi nchini humo, huku juhudi zaidi zikihitajika ili kuiinua nchi hiyo.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat