News

UGANDA: UMOJA WA DINI YA KIYAHUDI WAMPONGEZA MUSEVENI KWA KUMUONDOA IDD AMIN MADARAKANI.

on

Umoja wa dini ya KIYAHUDI nchini Uganda, maarufu Kama Abayudaya Jewish Community In Uganda, wamemshukuru Raisi Museveni kwa kumuondoa madarakani aliyekuwa Raisi wa zamani wa nchi hiyo, Iddi Amin Ddada.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa dini hiyo Rabbi Gershim Wambede katika maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa dini hiyo nchini Uganda.

Wambede amesema kuwa, aliyekuwa raisi wa zamani wa nchi hiyo Iddi Amin Ddada, alizuia kabisa uhuru wa kuabudu nchini Uganda, huku umoja wao ukididimizwa chini kutokana na sheria zilizowekwa kupinga uhuru wa kuabudu.

Alisema kuwa, katika kipindi cha utawala wa Raisi Amini, hawakuthaminiwa wala kujulikana kama walikuwepo, richa ya kwamba walikuwepo, na pia, serikali hiyo, ilitoa adhabu kali kwa wale waliojulikana kuwa walikuwa wakiabudu nje ya madhehebu matatu peke yake yaliyokuwa yakitambuliwa na serikali hiyo.

Wambede amesema kuwa, ni dhehebu la kiislamu, katoliki pamoja na Anglikan ambao walitambuliwa, lakini baada ya Raisi Museveni kumuondoa Iddi Amin na kuchukua madaraka alirejesha uhuru wa kuabudu na hapo ndipo heshima ilirejea

Naye waziri wa mazingira Bi. Mary Kitutu, aliyemwakilisha Spika wa wa bunge la Jamuhuri Ya Uganda, Bi. Rebecca Kadaga, aliwapongeza waumini wa dini ya kiyahudi kuwa ni miongoni mwa waumini ambao wamekuwa na msimamo wa amani na upendo katika jamii ya Uganda.

Pia Bi. Kitutu amewataka waumini hao, kuendelea kukiepusha na migongano ya kidini ambayo inaweza kusababisha kutoweka kwa amani ya kuabudu nchini humo.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat