News

DODOMA: TUNDU LISU AFUTIWA UBUNGE WAKE.

on

Spika wa bunge la Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bw. Job Ndugai, amesema, amemuandikia barua mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi NEC kumtaharifu kuwa wazi kwa kiti Cha ubunge Cha Jimbo la Singida Mashariki ambacho alikuwepo Tundu Lisu.

Spika Ndugai amesema kuwa; hii ni baada ya mbunge huyo wa Singida Mashariki kupotea katika bunge bila kuonekana, na bila taarifa yoyote ile, huku hata kambi ya upinzani ikishindwa kutoa taarifa rasmi juu yake.

Bwana Ndugai amesema, mbunge huyo kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lisu, hajaonekana katika vikao vya bunge kwa muda mrefu, na pia ameshindwa kujaza fomu ya tamko ya Mali na madeni.

Hivyo kwa kupotea bungeni bila taarifa na kutokuipata fomu yake ya tamko ya Mali na madeni, imemlazimu kutoa taarifa ya kuwa wazi kwa nafasi ya ubunge katika  Jimbo hilo na ikiwezekana NEC isaidie kupatikana kwa mbunge Jimboni humo

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat