News

JOHN CENA ATANGAZA KUSTAAFU MIELEKA.

on

Mwanamieleka maarufu duniani, John Cena amesema kuwa kwa sasa anafikiria kustaafu kucheza mchezo huo kwa kile alichodai kuwa umri unamtupa mkono.

John Cena akiwa uringoni tayari kwa pambano.

Cena mwenye miaka 42, akiongea na mtandao wa TMZ, amesema, amefikiria hivyo baada ya kutazama mchezo kati ya The Undertaker na Bill Goldberg mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita nchini Saudi Arabia.

Mchezo huo kati ya Taker na Goldberg uliwaboa mashabiki wengi wa mieleka baada ya mahasimu hao kuonekana wote wawili kuchoka mwanzoni mwa pambano hilo.

John Cena akitangazwa kuwa mshindi baada ya shindano.

John Cena amesema ameshangazwa na wanamieleka hao kucheza chini ya kiwango na anajiona na yeye anaelekea huko, hivyo haoni sababu ya kuendelea kucheza mchezo huo siku za usoni.

Hata hivyo, John Cena hajataja rasmi ni lini atatangaza kustaafu, lakini kutokana na majeraha yanayomuandama mara kwa mara huenda siku sio nyingi akatangaza adhma hiyo.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat