News

UGANDA: WILAYA 8 HATARINI KUPATWA NA EBORA.

on

Hofu imezidi kutanda katika wilaya mbalimbali za taifa la Uganda, baada ya maambukizi ya virusi vya ebora kudhibitika kuwapata baadhi ya watu nchini humo.

Watu 7 wanahofiwa kuwa na maambukizi hayo huku 3 wakithibitika kuwa na virusi hivyo ambapo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 amefariki kwa ugonjwa huo Jana Juni 11.

Waziri wa afya wa Uganda Bi. Ruth Aceng, amethibitisha kutokea kwa maambukizi hayo leo Juni 12, wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Kampala. Amesema kuwa; wilaya nyingi zimo hatarini kupatwa na janga hilo, ikiwa watu hawatajizatiti na kuzingatia kanuni mbadala za kukabiliana na gonjwa hili.

Bi Aceng, amezitaja wilaya za Kasese, Kabarole, Ntoroko, Bundibugyo, Bunyangabu, Kisoro, Kampala pamoja na Wakiso, kuwa ni miongoni mwa wilaya zilizopo hatarini kupatwa na maambukizi ya ebora kiurahisi.

Kutokana na mripuko wa gonjwa hilo katika wilaya ya Kasese, mpakani mwa Uganda na Kongo, wataalamu mbalimbali wa afya, wamepelekwa kuhakikisha usalama na vipimo vya wote wanaoingia nchini humo, huku shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) nchini humo, nalo pia limeingia katika jukumu la kuhakikisha usalama wa afya wa watu wote.

Ikumbukwe kuwa, hii sio Mara ya kwanza kwa taifa la Ugada kupatwa na maambukizi ya ebora, ambapo kila Mara, maambukizi hayo yameanzia mpakani mwa Uganda na Kongo.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat