News

SOWETO: MTOTO ALIYEZALIWA AIBIWA HOSPITALINI.

on

Kuibiwa kwa mtoto aliyezaliwa, inasemekana kuwa tukio hilo limetokea wakati wa mchana muda wa ziara.

Idara ya Afya ya Gauteng imethibitisha kwamba mtoto aliyezaliwa ameibiwa Alhamisi katika Hospitali ya Chris Hani Baragwanath huko Soweto.

Tukio hilo linadaiwa kuwa limefanyika wakati wa mchana muda wa kuzuru wagonjwa.

Picha za CCTV kutoka hospitali zinaonyesha mtuhumiwa wa kike anayezunguka na karibu na kliniki na baadaye akaonekana akiondoka eneo hilo, akibeba mtoto katika blanketi.

Ameonekana baadae akiwa na washirika wawili ambapo walionekana kubadili mablanketi kabla ya kuondoka hospitali.

Mpaka sasa mtuhumiwa anasakwa na Polisi.

Mkurugenzi wa Afya wa Gauteng Bandile Masuku wanasema wana matumaini, polisi wachukue hatua kwa haraka kumtambua mtuhumiwa.

“Sisi kwa kweli tumepokea habari za kusikitisha, habari za kuibiwa kwa mtoto aliyezaliwa Chris Hani Baragwanath. Pia tumetaarifu polisi. Tumewasilisha picha za CCTV kwao ili waweze kugundua kitu. Tunatarajia na kuomba kwamba alietenda hivo atatambulika na kwamba mtoto atarudi kwa mama kwa salama. “

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat