News

UGANDA: SITA WARIPOTIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA MAPOROMOKO YA ARDHI.

on

Watu 6 wameripotiwa kupoteza maisha, huku mamia wakibaki bila makazi katika maporomoko ya ardhi mashariki mwa Uganda.

Maporomoko hayo yametokea katika wilaya ya Bududa, mashariki mwa Uganda, usiku wa kuamkia leo na kusababisha madhara makubwa sana ambapo familia nyingi zimebaki bila makazi.

Hii ni kutoka na na mvua kubwa ambazo zilinyesha usiku wa kuamkia leo na kusababisha maporomoko makubwa ya ardhi ambapo watu sita wamepatikana wakiwa wamekufa na wengine wengi wakiendelea kutokujulikana walipo.

Bwana Godfrey Walenga, mbunge wa Bududa, amesema kuwa, ni masikitiko makubwa sana kutoka kwa tukio hilo maana watu wengi wameathirika kwa sababu wamewapoteza ndugu zao, huku wengi wao wakibaki bila mahali pa kujistiri kutokana na makazi yao kuchukuliwa na mvua.

Serikali ya Uganda imetoa pole kwa wahanga wa tukio hilo, huku jitihada za kuwahamisha wahanga zinaendelea ambapo msemaji wa serikali amesema kuwa, linahitajika eneo kubwa ili kuweza kuwahamisha watu wote katika eneo hilo maana madhara ya aina hii yamekuwa yakitokea Mara kwa mara na kuzidi kusababisha madhara makubwa.

Wilaya ya Bududa imekuwa ikiripotiwa kuwa na maporomoko ya ardhi, ya hapa na pale, na madhara yamekuwa yakitokea Mwaka hadi Mwaka ambapo serikali ya Uganda imebeba jukumu la kuhakikisha inawahamisha watu wote kutoka katika eneo hilo.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat