News

KAMPALA: SIKU YA MASHAHIDI WA UGANDA, MAELFU WAFIKA KUHIJI.

on

Tangu kuanza kwa mwezi Huu, maandalizi ya siku ya kumbukumbu ya mashahidi wa Uganda yalianza, huku wengi kutoka maeneo mbalimbali wakianza safari kuelekea Namugongo jijini Kampala, ambapo wengi wao walitembea kwa miguu hata kutoka nchi jirani.

Siku ya mashahidi wa Uganda, huadhimishwa mei 3, na Mwaka huu imetimia miaka 55 tangu mashahidi hao walipouawa kwa amri ya mfalme Mwanga II wa Buganda.

Mauaji hayo yalitokea wakati ambapo ufalme wa Buganda ulikuwa katika mgongano wa kisiasa pamoja na kidini, wakati ambapo kanisa Katoriki, Anglikan pamoja na dini ya Kiislamu, waliingia katika mgogoro wa nani ni mwenye nguvu zaidi.

Leo Juni 3, wakristo wa kikatoliki na wa kianglikan wamejumuika katika makumbusho ya mashahidi hao kwa ibada ya pamoja, kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaombea mashahidi wafia dini.

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na raisi wa Jamuhuri ya Uganda Gen. Yoweri Kaguta Museveni, wamefika katika makumbusho hayo kufikisha maombi yao mbele za MUNGU na kuliombea taiga LA Uganda.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat