News

KAMPALA: MAMA MARIA NYERERE AWAONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KATIKA HIJA NAMUGONGO.

on

Mamia ya wakristo wa Tanzania kutoka sehemu mbalimbali, wakiongozwa na aliyekuwa mke wa baba wa taifa, mama Maria Nyerere, wamejumuika pamoja na maelfu ya wakristo kutoka maeneo mbalimbali kwenye ibada za kumbukumbu ya mashahidi wa Uganda.

Akizungumza na jopo la watanzania katika maadhimisho hayo, raisi wa Jamuhuri Ya Uganda Gen. Yoweri Kaguta Museveni, amewashukuru watanzania na hasa mama Maria, kwa kujenga desturi ya kufika Namugongo kila mwaka katika maadhimisho hayo.

Raisi Museveni amesema, kila mwaka, mama Maria huwaongoza mamia ya mahujaji kutoka Tanzania, jambo ambalo limezidi kumuhakikishia kuwa, yeye si mwanadini tu, Bali ni kiongozi mcha Mungu, ambaye huwaongoza wengine katika njia ya Mungu.

Aidha, jopo la watanzania, wamepata nafasi ya kumuombea aliyekuwa baba wa taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kuzidi kuzikumbuka kazi zake njema alizozitenda kwa ajili ya Tanzania na bara zima la Afrika.

Na baadhi ya wanafunzi miongoni mwao, wamepata nafasi ya kuzungumza na raisi Museveni, na kumuomba kumzungumzia Mwl. Nyerere katika kitabu cha kihistoria wanachokiandika, ambacho kinayaelezea maisha na utumishi wa mwalimu Nyerere.

Kumbukumbu ya mashahidi wa Uganda, ufanyika kila mwaka Juni 3 katika eneo la Namugongo jijini Kampala, ambapo wakristo mbalimbali kutoka maeneo yote duniani, hujumuika katika ibaada ya hija na kumwomba Mungu.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat