News

KAMPALA: KAMANDA WA JESHI ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA USALITI WA NCHI YAKE.

on

Jeshi la wananchi nchini Uganda (UPDF) linamshikilia kamanda wake mmoja kwa tuhuma za kutoa taarifa za siri za ndani na kuzipeleka nchini Rwanda.

Kamanda huyo anayefahamika kama Paul Muwonge anashikikiwa katika kambi ya jeshi ya Makindye iliyopo jijini Kampala tangu 22/5 mwaka huu, baada ya kusadikika kushirikiana na jeshi la Rwanda na kulipatia siri hizo.

Hii ni kutokana na vuta n’kuvute ambayo imekuwepo kati ya taifa la Rwanda na Uganda, tangu mapema mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo nchi ya Rwanda ililazimika kufunga mipaka yake na Uganda kwa kuhakikisha hakuna mtu wala kitu chochote kutoka Uganda kuingia katika nchi ya Rwanda.

Bwana Muwonge ni mtuhumiwa hadi sasa, kutokana na kwamba hajapatikana na hatia yoyote hadi sasa, richa ya kwamba, baada ya kukamatwa, aliondolewa katika nafasi yake ya ucolonel ambayo alipewa kamanda mwenzake David Gonyi.

Hadi sasa haijafahamika vuta n’kuvute ya mataifa haya mawili itaishia wapi, kutokana na nchi ya Rwanda kuonekana kutokuwa tayari kuahirisha msimamo wake, richa ya upande wa Uganda kuwa kimya kwa muda sasa.

Chokochoko za hapa na pale za nchi ya Rwanda zimekuwa zikileta wasiwasi miongoni mwa watu wengi, richa ya kwamba upande wa Uganda umeweza kustahimili kishindo hadi sasa.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat