News

KAMPALA: MCHUNGAJI ASEMA LAZIMA KUTARAKIANA NA MKEWE.

on

Katika hali ya kushangaza, mchungaji wa kanisa la House Of Prayer Mchungaji Aloisious Bugingo amezidi kusisitiza kwamba lazima aachane na mke wake waliyeoana miaka 29 iliyopita na kutangaza kumuoa mke mwingine.

Kwa takribani wiki mbili sasa, imekuwa vuta nikuvute kati ya makanisa na wachungaji mbalimbali jijini Kampala, baada ya mchungaji huyo kutangaza hadharani kupitia redio na televisheni anavyo miliki (Salt FM na Salt TV) kwamba anataka kuachana na mkewe Teddy Bugingo ambaye ndiye mke wa ndoa na mchungaji kanisani hapo.

Richa ya jambo la kupeana taraka kwa wawili hao kuonekana ni ajabu kufanywa na wachungaji, kwake Mchungaji Bugingo imeonekana kuwa amedhamilia na kusema kuwa ni lazima amuoe mke mwingine.

Wakati anayasema hayo yote, mke wa mchungaji huyo amekataa kukubaliana na uamuzi wa mumewe, na kueleza kuwa, jambo hilo lipo kinyume kabisa na neno la Mungu, na ni aibu kwa wachungaji kufikia hatua hiyo.

Wachungaji mbalimbali wameupinga kwa kishindo uamuzi wa mchungaji huyo, na kusema, itakuwa ni aibu kwa kanisa na kwa watumishi wa Mungu, ikiwa familia ya mchungaji huyo itatengana.

Hadi sasa inaonekana kuwa, nguvu ya wachungaji hao imesababisha kupunguza makali na moto wa mchungaji Bugingo kutaka kumuoa mke mwingine, richa ya kwamba, kauli zake azitoazo kila siku, zinadhihirisha wazi kuwa amedhamilia kuutimiza uamuzi wake.

Mchungaji Teddy alioana na mchungaji Bugingo miaka 29 iliyopita na kujaaliwa kuwa na watoto 7 ambapo hadi sasa watoto wote wapo kwa mama yao ambapo inasemekana mchungaji huyo alihama toka nyumbani kwake na kuanza kuishi na binti ambaye inasemekana anataka kuoana naye.

Hadi sasa hakuna sababu maalumu ambayo imeelezwa na mchungaji Huyo kutaka kumuacha mkewe wa ndoa, zaidi ya tuhuma akizomuwekea mkewe kuwa anataka kuiba ardhi ya kanisa, tuhuma ambazo mkewe alizikana kupitia vyombo vya habari na kusema yeye hana nia ya kufanya hivyo na hati miliki zote anazo mumewe.

Kwa mujibu wa mke wake, mchungaji Bugingo, alianzisha migogoro hiyo miaka 4 iliyopita baada ya kuanzisha uhusiano na mmoja wa wafanyakazi wa kike wafanyao katika kituo chake cha habari, Richa ya kuwa mkewe alikaa kimya kwa kulinda ndoa yake pamoja na kanisa, na baada ya mumewe kutangaza hadharani na kumtuhumu, hakuwa na jinsi Ila kuieleza jamii ukweli wa mambo.

Haifahamiki ni nini hatima ya mgongano huo, lakini kutokana na maombezi ya wachungaji waliyoyaelekeza katika familia hiyo ili Mungu awarejeshe tena, imani ya watu walio wengi imekuwa ni kuiona familia hiyo ikiungana tena.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat