News

SUDANI: JESHI LAKATAA UTAWALA WA RAIA.

on

Jeshi la Sudani limekataa kukabidhi utawala kwa wananchi, wakati ambapo raia wa nchi hiyo wamekuwa wakiandamana kudai serikali irudishwe mikononi mwa raia.

Hii inatokea baada ya aliyekuwa raisi wa nchi hiyo Omar Al-Bashir kuondolewa madarakani mnamo tarehe 11 Aprili, baada ya kuitawala Sudani kwa miaka 30.

Raisi Bashir aliondolewa madarakani na balaza la mpito la jeshi, ambalo limechukua utawala kwa raia kwa kipindi cha miaka miwili, jambo ambalo halijakubalika kwa wananchi na hawapo tayari kukubaliana na hilo.

Afisa wa jeshi ngazi ya juu Lutenanti Generali Salah Abdilkhalek wa baraza la jeshi nchini humo amesema kuwa, hawatawaruhusu raia kuchukua nafasi za juu katika baraza la uongozi nchini humo katika kipindi hiki cha serikali ya mpito. Amesema kuwa, labda wanaweza kuzingatia kuwapa nafasi sawa za ujumbe katika baraza hilo.

Kwa sasa, raisi wa zamani wa nchi hiyo Bashir, amehamishiwa katika gereza la Kobar lililopo mji mkuu wa Kharloum baada ya siku kadhaa tangu amekamatwa na jeshi la Sudani.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat