News

MUSEVENI: NAFURAHIA LEO KUIONA UGANDA YA TOFAUTI.

on

Raisi Yoweli Kaguta Museveni ameyasema hayo jana 01 Mei, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi, ambayo imefanyika kitaifa katika wilaya ya Agago, Kaskazini mwa Uganda.

Raisi Museveni amesema kuwa, ni furaha isiyo kifani kuitazama Uganda iliyojaa amani na maendeleo, tofauti kabisa na miaka ya nyuma ambapo Uganda iliandamwa na vifo pamoja na mashambulizi ya hapa na pale, kama yale mauaji ya waasi yaliyo kuwepo Kaskazini mwa nchi hiyo, yale yaliyoongozwa na Joseph Kony.

Amesema kuwa, miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, umeme, reli na upatikanaji wa maji safi, ni moja ya nguzo zinazoweza kuupandisha uchumi wa nchi, hivyo amewataka wafanyakazi kuhakikisha ustadi wa utendaji kazi wao ili kuzidi kupanua wigo wa maendeleo nchini humo.

Pia raisi Museveni amewataka wafanyakazi kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unainuka, maana mshikamano ni muhimu sana ikiwa wanahitaji maendeleo katika sekta ya uchumi.

Aidha alisema kuwa, serikali ya Uganda imejitahidi kadri iwezavyo kupanua wigo wa ajira nchini humo, na kuwaahidi wafanyakazi kuwa, serikali haitachoka kuhakikisha nafasi zaidi za ajira zinapatikana ikiwa ni sambamba na malipo bora ya watumishi pamoja na pensheni kwa wastaafu.

Raisi Museveni, alipata nafasi ya kukagua shughuli mbalimbali za wafanyakazi kadri ya maandalizi yao na kusema kwamba inavutia sana kuwaona watu wenye moyo wa kulitumikia taifa lao.

Serikali ya raisi Museveni, imekuwepo madarakani kwa takribani miaka 33 sasa, na imejitahidi kuidumisha amani ya nchi hiyo kwa kipindi chote hicho.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat