News

MBEYA: JPM; BADO NAIKUMBUKA AHADI YA KUIPANDISHA MISHAHARA YA WATUMISHI.

on

Raisi wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewahakikishia wafanyakazi kuwa bado anaikumbuka ahadi yake ya kuipandisha mishahara ya wafanyakazi.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa hotuba yake kama mgeni rasmi, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika kitaifa jijini Mbeya nchini Tanzania.

“Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini, amenikumbusha ahadi yangu niliyoitoa mwaka jana kuhusu kuipandisha mishahara ya wafanyakazi, na ninazidi kusisitiza kwamba, sitaondoka madarakani bila kuitimiza ahadi hiyo.” Alielezea raisi Magufuli.

Aidha raisi Magufulu, amewataka wafanyakazi kuzidi kulijenga taifa, maana ni kupitia kwao, taifa linaimarika. Na aliongeza kuwa, serikali yake imepambana kadri ilivyoweza, kuyalipa madeni ya watumishi yaliyokuwepo, na hadi sasa, jumla ya bilioni 9.5 zilizokuwa zinadaiwa, tayari zimelipwa.

Serikali ya Tanzania iliyopo madarakani kwa sasa, ni moja kati ya serikali zinazo aminiwa kwa kutimiza ahadi ya yale yanayoahidiwa, na kutimiza majukumu yake sawa na neno lake.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat