News

DAR-ES-SALAAM: WAFUNGWA 3530 KUPEWA MSAMAHA WA RAISI.

on

Katika kusherehekea miaka 55 ya muungano was Tanganyika na Zanzibar, Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3530 ambapo 722 kati yao, wameachiliwa huru kutoka gerezani huku 2808 watabaki kumalizia sehemu ya kifungo chao.

Raisi Magufuli ameutoka msamaha huo leo Aprili 26 akitumia mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kati yao waliosamehewa ni pamoja na wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wagonjwa wa saratani, kifua kikuu pamoja na wale wanaoishi na viruai vya UKIMWI. Miongoni mwao pia kuna wanawake waliofungwa wakiwa wajawazito, walemavu wa mwili na akili, huku akiwataka wote kuthibitishwa na madaktari kabla ya kupokea msamaha huo.

Aidha, baadhi ya wafungwa hawakuhusika na msamaha huo, kutokana na makosa yao, ikiwa ni pamoja na wale wenye hukumu ya kunyongwa, makosa ya wizi, ubadhilifu wa fedha za serikali, waliokutwa na viungo vya binadamu, walio wakatisha watoto masomo, utekaji watoto pamoja na wale wanao tumikia kifungo kwa kutumia madaraka yao vibaya.

Hata hivyo, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imeahirisha sherehe za kusherehekea maadhimisho ya muungano kama ilivyokuwa desturi katika kuadhimisha Siku hiyo, na badala yake jumla ya milioni 988.9 za kitanzania zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe hizo, zitapangiwa shughuli nyingine za maendeleo ya taifa kama akivyoelezea jana waziri mkuu Kasim Majaliwa.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat