News

NEWS: KAMPALA – WATU KADHAA WAJERUHIWA KATIKA AJARI ILIYOHUSISHA MAGARI MANNE NA PIKIPIKI NNE.

on

Ajali mbaya iliyohusisha magari manne pamoja na pikipiki nne imetokea 24 April majira ya jioni katika eneo la Nakawa, wakati lori lenye mamba za usajiri UAA 497L lililokuwa likisafiri kutokea eneo la Ntinda kushindwa kusimama na kuyagonga baadhi ya magari na pikipiki zilizokuwa zikisubiri kuruhusiwa na taa za kuongozea vyombo vya moto barabarani.

Kati ya magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo, ni pamoja na magari madogo ya kubebea abiria, basi moja linalomilikiwa na kampuni ya Pioneer pamoja na magari mengine madogo mawili.

Msemaji wa jeshi la polosi jijini Kampala, Bwana Luka Owoyesigire, amesema kwamba, Jeshi la polisi linangojea taarifa kutoka hospitali kuu ya Mulago, ambako ndiko walipopelekwa majeruhi hao, ili kupata idadi kamili ya majeruhi hao na taarifa za afya zao.

Pia amesisitiza kuwa, polisi haiwezi kutoa taarifa ya kifo kwa sasa bila taarifa ya madaktari, hivyo inaweza kufahamika kwa sasa tu kwamba watu wote ni majeruhi.

Bwana Mbaaru Bashiri, mmoja kati ya watu waliokuwa waokoaji katika tukio hilo, amesema kwamba; amewaona watu wanne wakiwa tayari wamefariki, huku wawili wakiwa wanaume na wawili wakiwa ni watoto.

Pia aliongeza kuwa Richa ya hao wanne, kuna dereva wa gari moja la abiria pamoja na utingo wake ambao nao walipoteza maisha yao papo hapo.

Naweza kusema kwamba; jumla ya watu kama 10 wamepoteza maisha, maana huwezi kuniambia watu ambao vichwa vyao vimepondeka kiasi cha kushindwa kuwatambua, kwamba bado wapo hai. Aliongeza Bwana Mbaaru.

Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha taarifa hizo mpaka pale jeshi la polisi litakapotoa taarifa kamili juu ya wale wote waliopelekwa hospitalini.

Nawera Monica pamoja na Musinguzi Patrick ambao ni miongoni mwa walio salimika katika ajali hiyo, wamesema kuwa wamepona kwa neema ya Mungu tu, maana hakukuwa na ujanja wa kujiokoa wakati ajali hiyo ilipotokea.

Si mara ya kwanza kwa eneo hilo la Nakawa kupata ajali ya aina hiyo, kwani mwaka mmoja uliopita, ilitokea ajali iliyohusisha magari matatu yaliyogongwa na lori.

Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat