News

News: Onyesho la mwanamuziki Bobi Wine nchini Uganda kusitishwa na polisi.

on

Mbunge wa Kyadondo Mashariki na mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa na jeshi la polisi nchini humo, kutokana na kusitishwa kwa onesho lake la muziki, lililokuwa linatakiwa kufanyika leo katika ufukwe wa ziwa Victoria maarufu kama One Love Beach-Busabala.

Mapema Jana April 21, kamanda wa polisi Asumani Mugenyi, aliagiza kuzuiwa kwa maonyesho ya pasaka ya msanii huyo yaliyotakiwa kufanyika Arua, Kampala pamoja na Lira.

Aidha, jeshi la polisi limesema kuwa, onyesho hilo limesitishwa kutokana na msanii Huyo kushindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli hiyo, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na ulinzi wa kutosha katika eneo hilo ili kuhakikisha usalama wa watu.

Waandaaji wa maonyesho hayo, Anderew Mukasa pamoja na Abbey Musinguzi, nao wamekamatwa na jeshi la polisi mapema leo asubuhi, katika kituo kidogo cha polisi kilichopo One Love Beach-Busabala, na baadae kuondolewa katika eneo hilo.

Mashabiki na wafuasi wa msanii huyo, wametawanywa katika eneo hilo kwa mabomu ya machozi, huku baadhi yao wakikamatwa na jeshi la polisi kutokana na purukushani zilizokuwepo eneo la tukio kati ya polisi na mashabiki hao, wakati polisi ikijaribu kuwatawanya.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi, Bobi Wine amepelekwa na kuzuiliwa nyumbani kwake na haruhusiwi kujihusisha na shughuli yoyote ihusianayo na onyesho hilo.

  • Ikumbukwe kuwa, hii sio Mara ya kwanza kwa jeshi la polisi nchini humo, kufanya kitendo cha namna hii kwa msanii Huyo, kutokana na kilichotokea Desemba 26, 2018 katika eneo hilo baada ya polisi kuzuia onyesho alilokuwa ameliandaa, kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni kushindwa kukidhi vigezo.
Please follow and like us:
0

About Linuce Libent

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat