Politics

Chama tawala FLN kimeunga mkono Bouteflika aondolewe madarakani

By

on

Chama tawala nchini Algeria FLN kimeunga mkono kuondolewa adarakani kwa rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye ametajwa kuwa mgonjwa na hivyobasi kutoweza kuongoza.

Uamuzi huo wa FLN unajiri siku moja baada ya mkuu wa jeshi nchini humo Luteni Ahmed Gaed Salah kusema kuwa uamuzi wa kikatiba unafaa kufanywa kumuondoa afisini rais huyo.

Bouteflika ambaye yuko chini ya shinikizo kali baadaye alikubali kujiuzulu baada ya marekebisho ya kikatiba kupitishwa.

 

Mazungumzo yameanzishwa kujadili hatma ya siku za baadaye ya Algeria ambayo yataongozwa na mwanadiplomasia wa muda mrefu wa Umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi.

Maandamano yalianza mwezi mmoja uliopita wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aliposema kuwa anapanga kuwania urais kwa muhula mwengine .

Lakini watu waliendelea kuandamana hata baada ya kusema kuwa hatowania tena muhula mwengine na badala yake wakataka kufanyika kwa mabadiliko ya haraka.

Luteni jenerali Gaed Salah awali alinukuliwa akisema kuwa jeshi na raia wanafikiria kuhusu hatma ya taifa hilo akitoa ishara kwamba jeshi linaunga mkono maandamano hayo.

 

Katika hotuba ya mkuu wa jeshi wa Algeria Luteni Ahmed Gaed Salah, iliopeperushwa hewani katika kituo cha umma, kiongozi huyo wa jeshi na naibu wa wizara ya ulinzi alisema kuwa ‘‘katiba ndio njia pekee ya kuleta uthabiti wa kisiasa” .

Alitoa wito wa kutumika kwa kifungu 102 ambacho kinaliruhusu baraza la kikatiba nchini Algeria kutangaza wadhfa wa urais kuwa uko wazi iwapo kiongozi huyo hawezi kuongoza.

”Suluhu hii itavutia uungwaji mkono na lazima iungwe mkono na kila mtu” , aliaesma Luteni jenarali Gaed Salah ambaye alipongezwa na maafisa waliokuwa wakitazama hotuba yake.

Tangazo hilo la jeshi la Algeria ni muhimu sana.

Hatahivyo, hali ya afya ya rais Bouteflika, na mgogoro wa kikatiba kuhusu utawala wake hadi uchaguzi mwengine utakapofanyika mbali na wito wa waandamanaji ambao wanasalia katika barabara za Algeria, hatua hiyo haitarajiwa kufanikiwa.

 

Please follow and like us:
0

About admin

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat