News

News|Dudu baya akamatwa na polisi TZ

on

KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ anashikiliwa na Jeshi la Polisinchini Tanzania, katika Kituo cha Polisi cha Oyster Bay, jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki juzi nchini Afrika Kusini.

Lakini baadaye kupitia akaunti yake ya Instagram, Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.

Please follow and like us:
0

About Kelvin Zehot

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat