News

News| BASATA yawavaliya njuga Diamond na Rayvanny

on

Diamond na Rayvanny wamefungiwa kufanya onyesho la aina yoyote ndani na nje ya Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Baraza hilo limesema marufuku hiyo ya muda usiojulikana imeanza kutekelezwa Jana.

Wasanii hao wawili walikuwa hapo awali wametakiwa kuuondoa wimbo wao ‘Mwanza’ kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini wimbo huo umeendelea kuwepo kwenye YouTube.

Aidha, wameendelea kuucheza kwenye matamasha tofauti.

“BASATA imefikia maamuzi ya kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018, chini ya uongozi wake Diamond Platnumz,” taarifa ya Basata ambayo imetiwa saini na Onesmo Kayanda kwa niaba ya Katibu Mtendaji inasema.

“Pamoja na maelezo hayo, Baraza linatoa taarifa kuwa kibali cha Tamasha la Wasafi 2018 kimesitishwa kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini.”

Basata walitangaza kuufungia wimbo wa Mwanza mnamo 12 Novemba kwa kile walichosema ni “kwa kubeba maudhui machafu.”

“Lebo ya Wasafi, wasanii wake sambamba na vyombo vya habari vinapewa onyo na tahadhari kuendelea kutumia wimbo huu kwa namna yoyote ile,” baraza hilo lilisema.

Baraza hilo lilisema wimbo huo una “ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania” na kwamba umetumia “maneno yanayohamasisha ngono.

 

Baraza hilo wakati huo liliwaonga wasanii waliohusika, Rayvanny na Diamond, pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria na “kutoutumia wimbo huo na nyimbo nyingine zilizofungiwa kwa namna yoyote ile.”

Baraza hilo liliwataka “kuuondoa wimbo huo mara moja kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kufika saa kumi kamili” siku hiyo.

Taarifa hiyo ilitiwa saini na Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.

 

Diamond, taarifa zake kufungiwa zikisambaa, amepakia picha mbili kwenye Instagram akionekana kucheka na kufurahia sana akiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambapo kwenye kitambulisha mada amemwita ‘Kipenzi CHetu’.

 

 

Faini ya Tshs 3m

Siku moja baadaye, Basata walitoa taarifa na kueleza kuwa kikao cha Basata na wawakilishi wa Wasafi Limited ambacho kiliwashirikisha pia maafisa wa mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoka kwenye Kitengo cha Matukio na Uhalifu wa Kimitandao, kiliandaliwa kuujadili wimbo huo.

Basata walitoa maagizo zaidi ya kutolewa kwa wimbo huo kwenye YouTube na mitandao mingine haraka iwezekanavyo.

 

Diamond, Rayvanny na Wasafi Limited walitakiwa kila mmoja kulipa faini ya shilingi milioni tatu za Tanzania kabla ya siku 14 kupita.

“Kutokutekeleza ama kukaidi maagizo hayo kwa wakati uliopangwa kutapelekea Barazakuchukua hatua kali zaidi kwa wasanii hao na uongozi wao ikiwa ni pamoja na kuwafungia kabisa kujishughulisha na shughuli za sanaa nchini.”

 

 

Please follow and like us:
0

About Kelvin Zehot

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat