News

News| Mashoga afrika kusini waandamana mpaka ubalozi wa Tanzani

on

Wananchi wa Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria, Eastwood hapo jana, wakipinga vikali kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda uhamasishaji wa kuwaweka mbaroni wanaojihusisha na mapenzi ya jinsiya moja kwenye mkoa wake.

Wananchi hao wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini.

                                        Picha ya independent.co.uk (haihusiki na tukio)

Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu.

Tunakutaka uwape hifadhi watu hawa wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu” walisikika waandamanaji hao kwenye ujumbe wao.

Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini kitendo hiko kimekuwa kikipingwa na makundi mbali mbali ya haki za binadamu, wakisema ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Chanzo cha habari ALL AFRICA.COM

Please follow and like us:
0

About Kelvin Zehot

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat