Stories

Stories| Wajuwa kwanini muziki wa Burundi haupanuki kimataifa?

By

on

Tasniya ya muziki wa Burundi ina zaidi ya miaka 20, yaani tangu miaka ya elfu moja miya tisa na zaidi. Tasnia hii enzi za kale walikuwepo CANJO Amissi, Bahaga, Bruno SIMBAVIMBERE Gerard BUKURU, Geko nk… baadhi yao hatuona tena katika dunia hii. Wakongwe hao wengi wamestafu tasnia hii bila kuona matunda yake.
Leo hii katika kizazi kipya hiki bado tatizo lipo ila tofauti na muziki wa kale, sasa hivi kipato japo kidogo kipo japo hakiwezi ku kidhi mahitaji yao. wapo wasanii ambao kwa sasa wanafamilia zao (mke, watoto, mme) na wengine hulea hata wazazi wao na wadogo zao.

Wengi wao hawajishuhulishi na shughuli nyingine kama Biashara wala kazi mbadala za nje nje. maswali ni mengi kwa mashabiki wa muziki:
Je wanawezaje kuishi kwa kipato kidogo?
Je wanawezaje kuhudumia familia zao?
Swali ambalo kila siku huzuwa utata vichwani mwa watu ni pamoja na muziki wa Burundi ambao mashabiki wanadai kwamba haujikongoji au huwenda unatembea mwendo wa kinyonga.
Kwanini Muziki wa Burundi hautambuliki kimataifa kama muziki wa Nigeria, Tanzania, south Africa Nk…
Ni sababu Burundi hakuna Haki miliki?
mmoja kati ya wadau alifunguka na kusema ” Burundi ilitakiwa kuwa ya Pili katika kanda la Afrika Masharaki baada ya Tanzania, Licha yakufanya muziki mtamu wenye maufundi mengi, ila Burundi ni nchi ambayo raiya wake asilimia zaidi ya 60 wanazungumza kiswahili tofauti na Kenya, Uganda na Rwanda ila matokeo yake ni ya Mwisho baada ya Rwanda.”
mwingine amenieleza kuwa chanzo cha yote ni kuto kuwepo uhusiano mzuri kati ya wasanii, na endapo hali hiyo ikiendelea watajikuta hawafikii malengo.

Inafahamika kwamba wasanii wa Burundi ni mahodari kwa kucharaza muziki wenye ladha hasilia (Live Music) kwa kiingereza.
Maoni ya Wasomaji Ruhsa.

Please follow and like us:
0

About admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat