Politics

Politics| DRC: Je Martin Fayulu Mandindi ataungwa mkono?

By

on

Maandalizi ya uchaguzi nchini DRC yamepamba moto huku upinzani ukimtangaza Martin Fayuli Madidi kama mgombea wa pekee wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi unaopangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu, Kuna maoni tofauti kutoka kwa wananchi, wanasiasa na wachambuzi wa mambo ikiwa Martin Fayulu Madidi atapata uungwaji mkono wa kutosha wa kupambana na mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadari atakaegombea badala ya Raisi Joseph Kabila.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa alikua na haya ya kuzungumza na wafwasi wake:
“Mimi ni msemaji tu, msemaji wa mapambano, mapambano ya uhuru wa demokrasia tuliokuwa tukiitafuta miaka kadhaa na tunaelekea kwenye matokeo, ninashawishika na msaada wenu, msaada wa Mungu na msaada wa ushirika wetu na tutafikia matokeo ya mwisho kwa kusema kuifanya nchi yetu iwe ya kidemokrasia huru na inayojitegemea.”

Upande mwingine vinavyo muunga mkono Moïse Katumbi vinafurahia kutajwa kwa Martin Fayulu Madidi kuwa mgombea wa pekee wa upinzani na kumuunga mkoni, DRC imekumbwa na mzozo wa kisiasa kwa muda mrefu sasa, sambamba na maandamano yaliomtaka raisi Kabila kuondoka madarakani.

Please follow and like us:
0

About admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
WhatsApp chat